- 807 viewsDuration: 3:22Jioni hii, taifa jirani la Uganda linahesabu saa tu kabla ya kushiriki uchaguzi mkuu hapo kesho. Uchaguzi wa uganda umekumbwa na shutuma baada ya tume ya mawasiliano nchini humo kutangaza kuzimwa kwa mitandao hadi uchaguzi utakapokamilika. Sasa wanaharakati wanadai kuwa, hali hii inazima uhuru wa kujieleza wa raia wa uganda wakisema uchaguzi huo hautakuwa huru na haki