Skip to main content
Skip to main content

Mkenya anayebeba mimba kwa niaba ya wanawake wengione

  • | BBC Swahili
    17,481 views
    Duration: 2:01
    Je unaweza kukubali kumbebea mtu mwengine ujauzito au kubebewa mimba na mtu mwengine? Mtindo huu umeanza kushika kasi kama mojawapo ya suluhu zinazofaa zaidi kwa wanawake wenye matatizo ya uzazi. Kwa jina la kitaalamu 'surrogacy', ambapo kiinitete huundwa kwa kutumia yai la mama lililokusudiwa na mbegu za kiume za baba anayekusudiwa kisha kuhamishiwa kwenye mfuko wa uzazi wa mtu mwingine. Ingawa hii inazidi kupata umaarufu, nchi za Kiafrika hata hivyo hazina sheria zinazofaa za kuwalinda akina mama wajawazito na wazazi wanaowaagiza. Nchini Kenya, Ukosefu wa sheria juu ya kuasili imefanya iwe vigumu kwa wazazi kupata watoto wao kwa vile wanapaswa kupitia mchakato mgumu wa kuasili. Agnes Penda amezungumza na mwanamke anayefanya kazi ya kubebea wengine mimba na mtaalamu wa upandikizaji. @brianmala #bbcswahili #kenyantiktok #surrogacykenya Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw