Msafara wa Safaricom wa kusherehekea miaka 24 umeingia siku ya tatu

  • | Citizen TV
    244 views

    Msafara wa kampuni ya Safaricom katika maeneo mbalimbali nchini kusherehekea miaka 24 tangu ilipoanza kutoa huduma imeingia siku ya tatu. Msafara huo ukizuru kaunti ya Kericho na kuwatuza wakenya. Kuanzia Kericho, Chepseon, Kedowa hadi londiani wakenya walijishindia zawadi mbali mbali katika mpango wa “safaricom sambaza furaha”.