- 1,772 viewsMshukiwa wa mauaji ya mwanafunzi wa gredi ya sita Mercy Nyambura katika eneo la Njoro, Kaunti ya Nakuru, amekiri kuhusika na kifo chake. Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 16 amekamatwa leo na maafisa wa upelelezi. Kulingana na taarifa za uchunguzi, uchunguzi wa maiti umebaini kuwa marehemu alikumbwa na unyanyasaji na aliuawa, na uchunguzi zaidi unaendelea kubaini mazingira kamili ya tukio hilo.