- 1,249 viewsMsichana mwenye umri wa miaka 19 anaitaka Idara ya Polisi kuwajibika baada ya kudaiwa kupigwa risasi na afisa wa polisi wakati wa maandamano ya kupinga nyongeza ya bei ya mafuta. Sharon Nyambura anasema alipigwa risasi akiwa mtaani Kahawa West alipokuwa akisukwa nywele, wakati maandamano hayo yakiendelea katika eneo hilo. Sasa anadai haki na uwajibikaji kutoka kwa mamlaka husika, akisema tukio hilo limebadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa. Franklin Wallah ana taarifa zaidi.