Kulingana na msimamizi wa bajeti Margaret Nyakango, hazina ya kitaifa inazidi kuathirika na mirunduko ya madeni ambayo sasa imeanza kufikia kiwango cha kutozwa riba.
Nyakango anasema sasa malipo ya madeni hayo yanaathiri utekelezaji wa bajeti.
Nyakango...the debts that continue to attarct interests payments are now affecting budget implementation...
Nyakango ameiambia bunge kuwa kwa mwaka mmoja hazina ya kitaifa imelipa riba ya shilingi bilioni 53 ya kusawazisha madeni.
Nyakango..in 2025 alone we have paid upto 53 billion shillings as interests to three sets of debts alone....
Serikali ikiwa na deni la shilingi trilioni 6.6, msimamizi wa bajeti anasema kuwa taifa liko kwenye hali ya kupanda mchongoma na sasa kulipa deni ndio ngoma.