- 33 viewsMsongamano wa magari ulishuhudiwa kwa zaidi ya saa ishirini kwenye barabara kuu ya Nakuru kuelekea Eldoret. Msongamano huo ulienea kutoka eneo la Sobea, Mau- Summit hadi Timboroa. Maafisa wa usalama wanasema kuwa msongoamano huo ulichangiwa na gari moja kuharibikia barabarani. Na kama anavyoarifu Maryanne Nyambura, wasafiri waliolala barabarani wanasimulia mahangaiko yao.