Skip to main content
Skip to main content

Mtaa wa mabanda wa Upper Kathita Embu wasambaziwa umeme

  • | Citizen TV
    146 views
    Duration: 1:46
    Wakazi wa mtaa wa mabanda wa Upper Kathita katika eneo la Manyatta, Kaunti ya Embu, wamepata umeme baada ya kuishi gizani kwa miongo kadhaa kutokana na kukosa hati za umiliki wa ardhi. Kupitia mradi wa Last Mile Connectivity uliotekelezwa na Shirika la Usambazaji Umeme Vijijini (REREC) kwa ushirikiano na Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NG-CDF), maboma zaidi ya 100 yamenufaika na mradi huo. kulingana na wakazi, umeme umefungua fursa za biashara, kuboresha elimu na kuimarisha usalama katika eneo hilo.