- 8,312 viewsDuration: 31sVideo ya mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitatu, akining’inia nyuma ya lori zaidi ya kilomita 10 kutoka nyumbani kwao, imezua gumzo nchini Thailand. Video hiyo inaonyesha polisi wakilisitisha lori la kubeba barafu katika mkoa wa Sakon Nakhon, huku mtoto huyo akiwa bado nyuma ya lori hilo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya eneo hilo, mtoto huyo alimtoroka mama yake na kupanda kwenye lori bila dereva kugundua. Polisi walisema baadaye mtoto huyo aliunganishwa tena na wazazi wake. #bbcswahili #thailand #usalamabarabarani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw