- 653 viewsDuration: 2:30Familia moja huko Likoni, Mombasa, inamsaka mtoto wa miaka mitatu aliyetoweka nyumbani tarehe 20 Machi mwaka huu. Kulingana na ripoti ya polisi, jirani ambaye anadaiwa na familia kumuiba mtoto huyo, alionekana kuwa mjini Voi mara ya mwisho. Juhudi za kumtapa mshukiwa zimegonga mwamba huku wanaharakati Mombasa wakidai visa hivi vimeongezeka mno Mombasa.