- 8,788 viewsDuration: 3:46Mtoto wa tano aliyekuwa amesalia hai miongoni mwa pacha waliozaliwa na mwanamke mmoja kutoka Juja alifariki alipokuwa akipokea matibabu maalum katika Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta. Familia hiyo sasa inailaumu Hospitali ya Thika Level Five pamoja na KNH kwa madai ya utepetevu na kufeli kwa mifumo ya matibabu. Familia hiyo inasema mapungufu hayo yalichangia vifo vya watoto wote watano na kuikashifu KNH kwa madai ya kuwanyima huduma ya dharura. Na kama anavyoarifu mary Muoki, familia inadai madaktari walipoteza muda mwingi katika hospitali hiyo wakiwataka kwanza kuwasajili pacha hao kwa SHA ili wapate huduma.