Muokozi wa waraibu

  • | Citizen TV
    2,181 views

    Utumizi wa mihadarati umesalia changamoto kubwa si tu kwa serikali bali kwa familia nyingi za waraibu hawa. Tatizo la utumizi wa mihadarati mara nyingi huathiri watumizi na hata familia za wanaotumia dawa hizi kukidhi uchu wao na mara nyingi hata kusababishia familia nyingi umaskini. Lakini hata katika lindi hili la mihadarati, kuna wale ambao wamemudu kujinasua kutoka kwenye minyororo hii, na kama Brenda Wanga anavyoarifu, sasa wamejitahidi kusaidia kukabiliana na janga hili.