- 180 viewsKifo cha nduguye kutokana na uraibu wa dawa za kulevya kilimfungulia Monica Kilong’i ukurasa mpya kwenye maisha yake. Badala ya kukata tamaa, aliamua kuanza safari ya kuwaokoa waraibu wa pombe na dawa za kulevya Na kufungua kituo eneo la laini moja viungani mwa mji Wa Kitale. Monica ambaye ni muuguzi , sasa huzunguka mitaani kuwatafuta vijana, kuwapa mawaidha na kuwaelekeza katika vituo vya urekebishaji. Hebu tusikilize simulizi yake katika makala yetu ya mwanamke bomba.