- 276 viewsDuration: 1:52Muungano wa wajane unaitaka serikali kuanzisha hazina ya wajane ili kuwasaidia kuanzisha miradi ya maendeleo. Wakizungumza huko mombasa katika kongamano la kujadili baadhi ya changamoto zinazowakabili wajane, baadhi yao wakidai kutengwa na jamii. Mila potovu zikichangia pakubwa wao kuachwa nje katika miradi ya jamii wanazotoka na kutaka serikali kuwakumbuka wakisema wengi wao wamejipata wakiwachwa nje. Wanasema hazina hiyo itawawezesha kujikwamua kimaisha kama vile vijana na wazee ambao hupokea mgao wa serikali.