Katika harakati za kuendeleza ndoto ya babake kuhusu elimu, haswa kwa watoto walionusurika unyanyasaji na wanaotoka katika jamii zisizojiweza, ilimbidi Dkt Ruth Limo kuanzisha na kendeleza shule ya Edward Limo Educational centre huko Eldoret. Haikuwa rahisi kwake kama mwanamke kuendeleza urithi wa babake. Lakini kwa takriban miaka 10 sasa, anajivunia matunda ya uvumilivu na juhudi zake ambazo zimeifanya shule hiyo kukua na kutambulika. Ruth ndiye tunayemvisha taji kwenye makala ya leo ya Mwanamke Bomba. Hii hapa simulizi yake.