Skip to main content
Skip to main content

Mwanaume aliyepigwa na radi asimulia tukio la kutisha

  • | BBC Swahili
    7,857 views
    Duration: 1:18
    Mwanamume mmoja aliyepigwa na radi alipokuwa akitembea barabarani huko Staten Island nchini Marekani, ameelezea tukio hilo kuwa lilikuwa la “kutisha". Thomas Fahmy alisema alikuwa akitembea kuelekea kwa daktari wa meno Agosti 27 alipoona "mwanga mweupe unaong'aa" na papo hapo akaanguka chini. Alipelekwa hospitalini kwa msaada wa mkazi mmoja wa eneo hilo aliyewapigia simu huduma za dharura, na hakupata majeraha makubwa. #bbcswahili #marekani #radi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw