Skip to main content
Skip to main content

Mwanaume auawa na mwili wake kutupwa nje ya hoteli Tuuti

  • | Citizen TV
    2,096 views
    Duration: 1:23
    ‎Hali ya huzuni imetanda katika soko la Tuuti Kibabii katika Eneobunge la Kanduyi kaunti ya Bungoma baada ya mwanaume mmoja mhudumu wa hoteli kupatikana ameuawa. Kulingana na mmiliki wa hoteli hiyo Yusufu Majaliwa, Mfanyakazi wake alinaswa kwenye kamera za CCTV akianguka chini na kushuku kwamba alivamiwa usiku. ‎Wamelalamikia kudorora kwa usalama katika soko hilo, wakisema sio mara ya kwanza kuvamiwa wakiomba serikali kuingilia kati na kuboresha usalama. ‎