- 5,395 viewsDuration: 2:13Mwanaume mwenye umri wa miaka 29 anazuiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake katika eneo la Kimulot, Kaunti Ndogo ya Konoin, kaunti ya Bomet alfajiri ya Jumatatu. Kulingana na ripoti za polisi, mshukiwa anayejulikana kama Charles Korir kutoka kijiji cha Chepkitach, anadaiwa kumuua mpenzi wake Cynthia Chepkoech mwenye umri wa miaka 25 alipotaka kusitisha uhusiano wao. Maafisa wa polisi waliotembelea eneo la tukio walipata mwili wa marehemu ukiwa ndani ya nyumba ya mshukiwa. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa huenda marehemu alinyongwa . Inaarifiwa kuwa mshukiwa alijisalimisha mwenyewe katika Kituo cha Polisi cha Konoin, ambapo alikamatwa na kuwekwa kizuizini. Mwili wa marehemu umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Kapkatet ukisubiri upasuaji ili kubaini chanzo halisi cha kifo. Polisi wameanzisha uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo.