- 17,087 viewsDuration: 3:31Familia moja kutoka Bomachoge Chache, Kaunti ya Kisii inalilia haki baada ya mzee wa miaka 100 kuaga dunia kwenye mkanyagano uliotokea wanasiasa wakitoa pesa kwa waliokuwa wamehudhuria mkutano wa kisiasa eneo hilo. Familia hiyo inadai mzee huyo alikuwa miongoni mwa wakazi waliokuwa waking’ang’ania shilingi 200 kabla ya kukanyagwa na kufariki. Kisa hicho kilifanyika saa chache baada ya Rais William Ruto kuhutubia umma katika eneo hilo Jumatano wiki hii. Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Kisii anasema eneo la tukio lilikuwa mbali na mahali ambapo rais alihutubia wakazi.