Mwekezaji mmoja kutoka nchini Amerika,ametoa wito kwa asasi za uchunguzi pamoja na ubalozi wa Amerika humu nchini, kuingilia kati kile alichotaja kuwa njama kubwa ya ulaghai,ambayo imemgharimu mali ya thamani ya takriban shilingi milioni 89. Joel Fitzpatrick,ambaye sasa ni mkazi wa sehemu ya Watamu kaunti ya Kilifi,baada ya kufunga ndoa na mwanamke mmoja wa humu nchini,amesema aliwekeza fedha nyingi hapa nchini akitumai kuzindua biashara,kununua makazi pamoja na kuishi nchini na familia yake.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive