Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya, NACADA, imesema iko tayari kukabiliana na mbinu mpya zinazobuniwa na wasambazaji wa dawa za kulevya katika shule mbalimbali nchini.
Tamko hilo linajiri kufuatia ripoti zinazoonyesha kuwa walanguzi wa dawa za kulevya wameanza kutumia mbinu mpya na zinazobadilika kila wakati katika usambazaji wa mihadarati. Mbinu hizo kama kutumia biskuti na keki zinalenga kukwepa ufuatiliaji wa vyombo vya usalama, hali inayotajwa kuwa tishio kubwa kwa usalama wa umma.