Naibu gavana Mteule wa Uasin Gishu anaapishwa

  • | Citizen TV
    262 views

    Naibu gavana mteule wa kaunti ya Uasin Gishu Evans Kipruto anaapishwa hii leo kuchukua nafasi hiyo ya uongozi baada ya aliyekuwa Naibu wa gavana John Barorot kujiuzulu kutoka kwenye wadhifa huo. Kipruto alikuwa mwakilishi wadi kabla ya kuteuliwa na gavana Jonathan Bii na kuidhinishwa na bunge la kaunti ya Uasin Gishu kwa wadhifa huo.John Wanyama anaungana nasi mubashara kwa mengi zaidi.