- 7,358 viewsDuration: 1:50Naibu kinara wa ODM Abdulswamad Sharif nassir ametaka viongozi kutoka mrengo wa linda mwananchi kukoma kumrushia cheche za matusi kinara wa ODM Oburu Odinga akisema wengi ya wanachama wa ODM wanakubaliana na uongozi wake na kuwataka kuheshimu maoni ya wengi chamani. Akiongea huko Jomvu wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara amemtaka katibu Edwin Sifuna wao kuwa na msimamo kuondoka chamani akidai kuwa viongozi hao wamebuni chama akitetea viongozi wa ODM kutoka Pwani walioko serikalini kuhusu ajira kwa vijana,suala la ardhi pamoja na raslimali za umma.