- 471 viewsDuration: 1:45Wanachama wa UDA kaunti ya Taita Taveta wamemtetea naibu rais Prof. Kithure Kindiki wakisema nafasi ya unaibu rais ameifanya kwa ustadi mkubwa. Wakiongozwa na Idris Mohammed anayeongoza vuguvugu la "Kumi Bila Break" wanachama hao wanasema eneo la pwani litamuunga mkono Kindiki kuwa naibu wa rais kwa awamu ya pili ya rais William Ruto. Aidha wanachama hao wamesema kupitia ushirikiano wa rais na naibu wake eneo la pwani limepata miradi ya maendeleo hasa miradi ya barabara.