Naibu Rais Rigathi Gachagua atoa wito wa umoja wa viongozi Mlimani Kenya

  • | Citizen TV
    483 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua ameendeleza wito wa umoja wa viongozi wa Mlima Kenya, huku migawanyiko ikiendelea kudhihirika miongoni mwao. Akiongoza hafla ya kuchangisha pesa katika kaunti ya Meru, Naibu Rais pia ameonya kuhusu mzozo wa uongozi unaoendelea katika kaunti hii kati ya Gavana Kawira Mwangaza na wawakilishi wodi. Naibu Rais Gachagua akisema, ofisi yake haitaingilia mzozo huo akiwataka viongozi wenyewe kutafuta suluhu. Wakati huo huo, Naibu Rais pia ameendelea kuonya madalali wanaotatiza sekta ya kahawa Mlima Kenya