Naibu wa Rais William Ruto aikashifu serikali anayoihudumia kwa ongezeko la gharama ya maisha

  • | KTN News
    1,140 views

    Naibu Rais William Ruto na kikosi chake cha Kenya Kwanza wameendeleza kampeni yao katika eneo la Pwani hii leo wakiwa katika uwanja wa Tononoka. Ruto ameikashifu serikali anayoihudumia kwa ongezeko la gharama ya maisha. Akijitoa lawamani Ruto amelaumu salamu za heri baina ya Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga kama ndio chanzo cha ugumu wa maisha.