- 539 viewsAbiria nchini wamelazimika kulipa nauli za juu licha ya washikadau wa sekta ya matatu kutangaza kudumisha nauli katika viwango vya chini huku mazungumzo ya kutafuta suluhu yakiendelea. Pitapita katika stendi mbalimbali jijini Nairobi zimebaini kuwa bei zimepanda kwa hadi asilimia 50, kama ilivyotangazwa na baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri.