- 272 viewsDuration: 1:00Tume ya uwiani na utangamano nchini NCIC inaisihi bunge kuidhinisha mswada wa marekebisho ya sheria za NCIC ili kuipa tume hiyo mamlaka ya kuwakamata na kuwafikisha kortini wanaohusishwa na matamshi ya chuki na uchochezi.Afisa mkuu Dkt. Daniel Giti anasema licha ya tume hiyo kuwahoji wahusika, kuchunguza na kuwasilisha faili kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma, inachukua muda mrefu sana kwa wahusika kukabiliwa kisheria.