- 8,311 viewsDuration: 31sWenza hawa nchini Ufilipino waliamua kuendelea kufunga ndoa yao kanisani licha ya eneo hilo kujaa maji kutokana na mvua kubwa na mafuriko. Lhiane Galang na Gilbert Gibo Chico walilazimika kutembea kwenye maji yaliyofika hadi mapajani ili kufika kanisani na kufunga ndoa huko Hagonoy, pwani ya Manila. Umeme ulikuwa umekatika, hivyo kanisa lilitumia spika inayobebeka. Ingawa walishauriwa kuahirisha harusi yao kwa sababu ya hali hiyo lakini wao waliamua kutekeleza mipango yao kama walivyopanga. Mvua za msimu zilizokuwa kubwa kuliko kawaida zilisababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko ya ghafla, na kusababisha vifo vya watu 34. #bbcswahili #ufilipino #manila Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw