- 592 viewsDuration: 2:38Wakazi wa Sweetwaters katika Kaunti ya Laikipia wameelezea wasiwasi wao kutokana na uvamizi wa mara kwa mara wa ndovu ambao wamesababisha hasara kubwa ya mazao yao mashambani. Kwa mujibu wa wakazi hao, ndovu hao huvamia mashamba yao kila siku majira ya saa mbili asubuhi, wakiharibu na kula mazao yote. Wanasema hali hiyo imeendelea kwa takriban miaka miwili sasa, jambo lililowaacha wengi wao wakihangaika .