NHC inakabidhi mradi wa nyumba kwa kaunti ya Taita Taveta

  • | Citizen TV
    261 views

    Shirika la kitaifa la ujenzi wa Nyumba la NHC limekabidhi rasmi serikali ya kaunti ya Taita Taveta mradi wa nyumba za mbela katika eneo la Wundanyi baada ya serikali ya Gavana Andrew Mwadime kulipa deni la shilingi milioni 20 lililokuwa likidaiwa na shirika hilo. Hatua hii inajiri wakati serikali 26 za kaunti zikiwa bado zinadaiwa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwenye miradi sawia na shirika hilo la NHC