__ Watalii wanamiminika katika bustani ya mandhari ya kale ya Henan huku idadi ya wageni wakati wa likizo ikiongezeka.
///
Wakulima Nchini China Wakumbatia Teknolojia Mpya Kuanzia Umwagiliaji hadi Mauzo.
///
Mahitaji Makubwa Sekta Zinazoibukia Yaongeza Maagizo ya Mashine za Viwandani China.
///
Utalii wa kitamaduni wa kuzama moja kwa moja katika uzoefu (immersive cultural tourism) umekuwa kivutio kikubwa katika mji wa Kaifeng, katikati mwa mkoa wa Henan nchini China, ambapo umati wa hadi watu 90,000 kwa siku hutembelea Millennium City Park ili kushuhudia maonyesho yenye mandhari ya enzi ya nasaba ya Song pamoja na programu shirikishi za urithi wa kitamaduni.
Khamis Darwesh anaripoti.
///
Wakulima kote China wanazidi kutumia teknolojia mpya katika shughuli za kilimo. Kuanzia mifumo ya kisasa ya umwagiliaji hadi mauzo kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni, teknolojia inabadilisha namna mazao yanavyozalishwa na kuuzwa.Ronald Mutie anaripoti.
///
Watengenezaji wa mashine za viwandani nchini China wameongeza uzalishaji kwa kasi kubwa ili kukidhi ongezeko la maagizo, yanayosukumwa na mahitaji makubwa kutoka sekta mpya kama roboti zinazofanana na binadamu na magari mapya yanayotumia nishati mbadala (NEV) tangu mwanzoni mwa mwaka 2026.Jacob Mogoa anaripoti zaidi.
///
Ripoti mpya inaonyesha kuwa uchumi unaohusiana na huduma na mahitaji ya wazee, unaojulikana kama “silver economy”, unazidi kuwa chanzo kipya cha ukuaji wa uchumi nchini China. Hii inatokana na kuongezeka kwa idadi ya wazee nchini humo, ambayo sasa imefikia takribani watu milioni 320. Tom Wanjala na maelezo.
///
China imepiga hatua nyingine kubwa katika sekta ya usafiri baada ya treni yake mpya ya kasi aina ya CR450 kufikia mwendo wa kilomita 450 kwa saa wakati wa majaribio.
Mafanikio hayo yanaonyesha azma ya taifa hilo kuimarisha teknolojia ya kisasa na kuendeleza sekta ya viwanda kupitia ubunifu.Simiyu Wanjala anakamilisha taarifa hiyo.
///
Ifahamu China
Ukuaji wa vituo vya data vya Akili Bandia (AI) na miundombinu ya nguvu za kompyuta nchini China unafungua fursa mpya kwa sekta ya nishati ya jadi. Mabadiliko haya pia yanaongeza mahitaji ya vifaa na kuchochea ubunifu katika sekta hiyo.
////
Jifunze Kichina
Naam, mtazamaji, sasa ni wakati wa sehemu yetu ya Jifunze Kichina! Katika sehemu hii, tunawaletea masomo ya lugha ya Kichina, hatua kwa hatua, kwa njia rahisi na ya kuvutia. Karibu tujifunze pamoja.
Thank you for watching this video. Kindly subscribe for more content from 'Home of The Untold Stories.'
*About TV47*
'TV47 is on GOtv (Channel 102), DStv (Channel 268), SIGNET, Gotv, BAMBA and STARTIMES.
__
For Breaking News, kindly subscribe by sending ‘NEWS’ to 22047.
__
Connect with us:
Website: https://www.tv47.digital/
Facebook: https://www.facebook.com/TV47KE
Twitter: https://twitter.com/tv47news
Instagram: https://www.instagram.com/tv47ke/
TikTok: https://www.tiktok.com/@tv47_ke
Telegram: https://t.me/tv47_ke
WhatsApp: 0797 047 047
__