CHINA YAJENGA MTANDAO MKUBWA WA MAJI DUNIANI KUSAIDIA MAENDELEO YA KISASA
///
CHINA YAFIKISHA ZAIDI YA VITUO MILIONI 21 VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME
///
ZIARA YA KITAMADUNI YA IJUE CHINA YAANI “DISCOVER CHINA 2026” YAZINDULIWA RASMI, MABALOZI WA NJE WAANZA SAFARI YA KUIFAHAMU CHINA KWA UNDANI
////
China imeendelea kupiga hatua kubwa katika kuimarisha usalama wa rasilimali za maji baada ya kujenga mtandao wa kitaifa wa maji unaotajwa kuwa mkubwa zaidi duniani.
Mtandao huo unahusisha mabwawa, mifumo ya usambazaji na miradi ya kuhamisha maji kati ya maeneo mbalimbali, hatua inayolenga kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa mamilioni ya watu pamoja na kusaidia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii nchini humo.
Simiyu Wanjala anaarifu zaidi.
/////
Miundombinu ya kuchaji magari ya umeme nchini China imeendelea kukua kwa kasi, huku idadi ya vituo vya kuchaji ikifikia zaidi ya milioni 21. Kama anavyotueleza Tom Wanjala, ukuaji huu unaonyesha namna matumizi ya magari ya umeme yanavyoongezeka kwa kasi nchini humo.
////
Ziara ya Kitamaduni ya Discover China 2026 yaani Ijue China imeanza rasmi siku ya Ijumaa jijini Beijing, ikiwaleta pamoja zaidi ya wageni 200 wakiwemo mabalozi kutoka nchi 40 pamoja na wawakilishi wa sekta mbalimbali ndani na nje ya China. Washiriki hao wataanza safari maalum ya kuchunguza mandhari, utamaduni na maendeleo ya nchi hiyo. Jacob Mogoa anaripoti zaidi.
/////
Mpango maarufu wa mafunzo ya ufundi kutoka China unaendelea kupanua wigo wake barani Afrika, ukivuka sekta za jadi na sasa kuingia kwa kasi katika ulimwengu wa teknolojia ya kidigitali. Warsha za Luban, mpango wa China wa kutoa mafunzo ya kitaaluma nje ya nchi, kwa miaka kadhaa zimekuwa daraja muhimu la ubunifu na maendeleo ya ujuzi kati ya China na Afrika. Zimepewa jina la fundi stadi wa kale wa China, Lu Ban, na zinawakilisha mfano wa ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote katika elimu ya ufundi.
///
Kwenye sehemu yetu ya Ifahamu China leo Zakia Peng anatufahamisha jinsi mwalimu kijana wa shule ya msingi kusini magharibi mwa China anatumia dansi za mtaani kuwajengea wanafunzi wake kujiamini, hasa wale wanaoishi mbali na wazazi wao au kutoka katika familia zilizovunjika.
///
Jifunze Kichina
Naam, mtazamaji, sasa ni wakati wa sehemu yetu ya Jifunze Kichina! Katika sehemu hii, tunawaletea masomo ya lugha ya Kichina, hatua kwa hatua, kwa njia rahisi na ya kuvutia. Karibu tujifunze pamoja.
__
Thank you for watching this video. Kindly subscribe for more content from 'Home of The Untold Stories.'
*About TV47*
'TV47 is on GOtv (Channel 102), DStv (Channel 268), SIGNET, Gotv, BAMBA and STARTIMES.
__
For Breaking News, kindly subscribe by sending ‘NEWS’ to 22047.
__
Connect with us:
Website: https://www.tv47.digital/
Facebook: https://www.facebook.com/TV47KE
Twitter: https://twitter.com/tv47news
Instagram: https://www.instagram.com/tv47ke/
TikTok: https://www.tiktok.com/@tv47_ke
Telegram: https://t.me/tv47_ke
WhatsApp: 0797 047 047
__