- 310 viewsMdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakango, amerejea mahakamani kutafuta ufafanuzi kuhusu iwapo serikali za kaunti zinaweza kuendelea kutoa basari. Nyakango anataka ufafanuzi wa dharura wa mahakama kuhusu iwapo maombi ya magavana ya fedha za ufadhili wa masomo kwa mwaka wa kifedha wa 2026/2027, yanafaa kuidhinishwa au la. Mahakama ilisitisha utoaji wa basari mwezi Juni baada ya kubainika kuwa basari za kaunti ni kinyume na Katiba.