Skip to main content
Skip to main content

Nyumba 70 zapeperushwa na kimbunga Chile

  • | BBC Swahili
    7,243 views
    Duration: 22s
    Kimbunga kilichoukumba mji wa Requínoa, katika eneo la O’Higgins katikati mwa Chile, Jumatatu, Oktoba 26, kimesababisha uharibifu wa takriban nyumba 70 na shule moja. Nguzo za umeme zilizoanguka na nyaya zilizokatika zilisababisha kukatika kwa umeme kwa karibu watu 3,000, huku mtu mmoja akiripotiwa kujeruhiwa kwa majeraha madogo. Mamlaka ya kukabiliana na majanga ilitangaza tahadhari nyekundu katika eneo hilo na kupeleka timu za uokoaji kusaidia waathirika, wakati shughuli za kuondoa vifusi zilizokuwa zimeziba barabara zikiendelea. Ingawa vimbunga si vya kawaida nchini Chile, vinapotokea mara nyingi huathiri maeneo ya kusini-kati mwa nchi. Kwa kawaida, hutokea kati ya Mei na Agosti, kipindi cha majira ya vuli na baridi. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw