- 2,501 viewsDuration: 2:48Katibu wa usalama wa ndani Raymond Omollo sasa ametoa onyo kwa viongozi wa kisiasa dhidi ya kutozingatia sheria kabla ya mikutano yao. Akizungumza huko Kisumu, Omollo alisema kuwa sharti kila mmoja afuate sheria za mikutano ya hadhara ili kuzuia mikwaruzano na serikali. Haya yanajiri huku baadhi ya viongozi wakidai kuwa serikali haiwajibiki katika kuchukua hatua dhidi ya wahuni, huku wakimtaka Katibu Omollo ajiuzulu.