- 61,094 viewsDuration: 1:32Kiongozi wa kanisa la dhehebu tata nchini Kenya, Paul Mackenzie, amehukumiwa kifungo cha miaka 200 jela na Mahakama Kuu ya Mombasa kwa mauaji ya watu 191, wote isipokuwa mmoja wakiwa watoto. Mackenzie pamoja na wafuasi wake zaidi ya 20 walikutwa na hatia ya kuendesha mfumo uliopangwa ndani ya Msitu wa Shakahola, ambapo waliwaelekeza wazazi kuwanyima watoto wao chakula hadi kufa, wakidai kwamba walikuwa wakifanya hivyo ili “wakutane na Yesu.” Mackenzie, aliyejitambulisha kama mchungaji, alikamatwa mwaka 2023 baada ya kugunduliwa kwa zaidi ya miili 400 katika makaburi yasiyo na kina ndani ya Msitu wa Shakahola, karibu na pwani ya Kenya. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw