- 265 viewsDuration: 1:49Wafanyibiashara wa bodaboda eneo la Bahati kaunti ya Nakuru, wametakiwa kujisajili Katika makundi Yao ya kazi kama njia moja ya kupambana na visa vya utovu wa usalama Katika eneo hilo. Wakizungumza Katika mkutano wa usalama uliowaleta pamoja maafisa wa polisi Katika eneo Bahati, Viongozi wa bodaboda kutoka wadi tano za eneo Bunge hilo, na maafisa kutoka ofisi ya Mbunge wa eneo hilo wamesema ipo haja ya ushirikiano wa sekta zote Kwa kuimarisha usalama Kati Yao..