Polisi Sultan Hamud waandaliwa hafla ya Krismasi na mwanajeshi mkongwe

  • | Citizen TV
    3,242 views

    Maafisa wa polisi kutoka kituo çha sultan hamud kaunti ya makueni wametabasamu baada ya kuandaliwa karamu siku moja baada ya sikukuu ya krismasi kwani wengi wao walikosa kujiunga na familia zao kwa sherehe hizo kutokana na sababu za kikazi Muandalizi wa sherehe hiyo meja mstaafu Shedrack Muiu anasema alichukua hatua hiyo kama njia mojawapo ya kuwakumbuka polisi ambao wako mbioni kuhakikisha usalama unadumishwa wakati wananchi wengine wanapojumuika na familia zao kuadhimisha sikukuu ya krismasi. Aidha meja huyo mstaafu ametoa changamoto kwa wakenya kuwa wakarimu kwa maafisa wa polisi akisema majukumu wanayotekeleza maafisa hao ya kudumisha usalama ni muhimu kwa jamii.