Maafisa wa polisi katika Kaunti ya Nandi wamefanya msako mkali katika maeneo ya bondeni mjini Nandi na kufanikiwa kusambaratisha mtandao wa utengenezaji wa pombe haramu uliokuwa ukiendeshwa kando ya mto.
Operesheni hiyo ya kushtukizia iliongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nandi, Samuel Mukuusi, ambaye aliongoza kikosi chake hadi kwenye kambi hizo zilizofichika ambapo watengenezaji sugu wamekuwa wakitengeza pombe hiyo kwa wingi. Wakati wa oparesheni hiyo, polisi walifanikiwa kuwanasa washukiwa watatu.