- 3,170 viewsDuration: 3:26Dakika za mwisho za marehemu Rex Kanyike Masai zilisimuliwa upya mahakamani hii leo wakati rafiki yake wa karibu, alipotoa ushahidi katika uchunguzi unaoendelea na ambao umechukua takriban miaka miwili sasa. George Ndikas aliieleza mahakama kuwa maafisa wa polisi walifyatua risasi kila upande kabla ya risasi kumlenga Rex. Ndikas akisema kuwa alisikia milio mitatu ya risasi, moja iliyompata masai katika paja la kushoto.