- 18,041 viewsDuration: 1:05Rais William Ruto kwa mara nyingine amemsuta aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua kwa madai ya kuipokonya familia ya marehemu kakake mali yao. Rais amesisitiza kuwa atahakikisha familia ya marehemu nderitu gachagua inapata haki. Suala hili limegonga vichwa vya habari kwa juma moja sasa huku viongozi serikalini wakiendelea kumshambulia rigathi gachagua kwa madai ya kudhulumu familia ya nduguye. Madai hayo yameshinikizwa na hatua ya familia kumuandikia Rais Ruto wakitaka aingilie kati. Hata hivyo Gachagua amesisitiza kuwa familia haikupunjwa na kwamba nduguye alikuwa ametoa wosia wa urithi ambao ulitekelezwa na mahakama kikamilifu.