Rais Wiliam Ruto aliendelea na ziara yake katika eneo la Nyanza, akipiga kambi katika kaunti ya Migori, ambapo aliipongeza serikali jumuishi kuwa muungano pekee wa kisiasa wenye mpango wa kulibadilisha taifa hili kuelekea kwenye kilele cha ustawi. Rais Ruto aliukashifu upinzani, akisema unashirikisha viongozi wanaoongozwa na uovu na chuki wakiwa hawana mpango wa sasa au maono ya mustakabali kwa ajili ya taifa hili. Kiongozi wa taifa aliwaambia wakazi wa Migori kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka ujao utahusu kura ya umoja.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive