- 1,197 viewsDuration: 1:34Rais William Ruto ametetea ndoto yake ya kubadilisha Kenya kutoka kwa viwango vya mataifa maskini hadi kufikia mataifa tajiri zaidi duniani, akisema wakenya wana nafasi na rasilmali ya kutosha kubadilisha Kenya kwa miaka 10 ijayo. Akizungumza katika eneo la Lodwar Kaunti ya Turkana leo, Rais Ruto aliwakashifu viongozi wa upinzani ambao wamekashifu mpango huo, akiongeza kwamba viongozi hao hawana maono.