Rais Ruto amesema hatakaa Kimya Maandamano Yakivuruga Amani

  • | Citizen TV
    3,531 views

    Rais William Ruto amesisitiza kwamba hatakaa kimya na kushuhudia vifo, ubakaji na uharibifu wa mali wakati wa maandamano. Rais Ruto amesema kuwa Katiba inamtaka kulinda maisha na riziki ya Wakenya. Aidha, Rais ametetea rekodi yake ya ajira, siku moja baada ya kuwataka polisi kuwapiga risasi miguuni na kuwajeruhi wahuni. Rais alikuwa akizungumza alipokuwa mwenyeji wa mabingwa wa Ligi ya Kitaifa ya Daraja la Pili, Nairobi United FC, katika Ikulu ya Nairobi