- 4,408 viewsDuration: 3:04Katika kila hatua ya kuagiza bidhaa kutoka mataifa ya kigeni, jina la matapeli si geni katika vinywa vya wanasiasa na viongozi nchini. Katika kashfa ya punde zaidi kuhusu uagizaji wa mafuta, Rais William Ruto aliwafokea na kuwaonya wahusika wa sakata hiyo, akiwataja kuwa matapeli. Jina matapeli kuwa wahusika wakuu wa sakata mbalimbali limeandika historia katika sakata kubwa za mafuta, mahindi, mchele na hata mbolea.