Rais William Ruto pamoja na rais wa Msumbiji Daniel Chapo hii leo wameongoza kongamano la uwekezaji katika hoteli moja hapa jijini Nairobi. zaidi ya kampuni 20 zimeafiki kuwekeza zaidi ya dola bilioni 2.9 katika sekta mbali mbali nchini ikiwemo afya, kilimo na madini. Rais Ruto ametumia fursa ya kongamano hilo kuwashukuru wawekezaji akisema kenya iko tayari kwa shughuli za uwekezaji na kwamba raia wa kenya wanauwezo na fursa bora zaidi ulimwenguni kushiriki katika uwekezaji. Kaunti kadhaa kama vile Kilifi, Nairobi, Tana river, Kitui miongoni mwa kaunti nyingine.