- 1,233 viewsDuration: 2:59Rais aanza ziara hiyo kwa kutoa hati miliki 33,000 katika hafla iliyoandaliwa katika bustani ya mama ngina kaunti ya Mombasa. Rais Ruto asema kuwa hatua hiyo itatoa tiba ya uskwota katika kaunti za mombasa, Kilifi, Tana River, Taita taveta na lamu. Rais ruto aidha ameitaka wizara ya ardhi kutoa ati miliki 200,000 zaidi kwa kipindi cha miezi mitatu ili kuzika katika kaburi la sahau shida ya mashamba katika eneo zima la Pwani.