- 2,982 viewsDuration: 3:09Rais William Ruto amesema serikali yake itarekebisha makosa ya zamani yaliyochangia ubaguzi dhidi ya Wakenya wanaoishi eneo la Kaskazini Mashariki, huku akiwaahidi wakazi wa maeneo hayo haki na usawa katika huduma za serikali. Rais, aliyezuru kaunti ya Mandera, aliwataka wakazi kujisajili kupata vitambulisho ili waweze kupata huduma za serikali. Akisema kuondolewa kwa msasa kwa wakazi kumeondoa vikwazo vilivyowatenga Wakenya wengi wanaoishi katika maeneo ya mipakani.