Skip to main content
Skip to main content

Ruto aomba msamaha kwa ubaguzi wa Kaskazini mwa Kenya

  • | Citizen TV
    726 views
    Rais William Ruto ameomba msamaha kwa niaba ya serikali kutokana na kile alichokitaja kuwa ubaguzi wa muda mrefu dhidi ya maeneo ya Kaskazini mwa Kenya chini ya tawala zilizopita. Akihutubia taifa wakati wa sherehe za Madaraka Dei katika Kaunti ya Wajir, Rais alisema anasikitishwa na hali hiyo na kuahidi kuwa serikali yake itaweka juhudi za makusudi kurekebisha changamoto zilizodumu kwa miongo kadhaa. Rais alisema hatua hizo zitajumuisha uwekezaji mkubwa katika miundomsingi, elimu, afya na sekta nyingine muhimu ili kuhakikisha eneo hilo linapata maendeleo sawa na sehemu nyingine za nchi. Mwanahabari wetu Sam Gituku alihudhuria hafla hiyo na anatuletea taarifa kamili.